MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya ligi inaendelea leo kwa michezo tisa ukiwemo wa kinara wa ligi hiyo Liverpool itakayokuwa mgeni wa Girona ambayo imeandika katika mitandao yake ya kijmaii “A big match in an incredible city! Welcome to Girona, @liverpoolfc 👋”.
Liverpool inaongoza ikiwa na pointi 15 baada ya michezo mitano wakati Young Boys ipo nafasi ya mwisho katika msimamo wa timu 36 zinazoshriki haina pointi.
Michezo mingine inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Dinamo Zagreb vs Celtic
Atalanta vs Real Madrid
Bayer Leverkusen vs Inter
Brest vs PSV Eindhoven
Club Brugge vs Sporting CP
RB Leipzig vs Aston Villa
RB Salzburg vs Paris Saint-Germain
Shakhtar Donetsk vs Bayern Munich