Kasekenya: TBA zingatieni ubora wa majengo

WAKALA wa Majengo nchini (TBA) wametakiwa kuzingatia ubora na ufanisi wa majengo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi
na uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alipokuwa akikagua jengo la ghorofa sita kwa ajili ya makazi ya watumishi wa umma linalojengwa mtaa wa Ghana Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Jengo hilo litagharimu Sh bilioni 7.

Advertisement

7

Kasekenya amewataka TBA kuzingatia ubora na ufanisi wa majengo katika ujenzi wa nyumba mpya za watumishi zinazoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aidha Kasekenya ameagiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ya Mwanza kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha zinakamilika kwa wakati na katika ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake kaimu meneja TBA Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Mosses Urio amesema gharama za mradi ni Sh bilioni 7 ambapo unatarajia kukamilika ifikapo July 2024.

Mhandisi Urio amesema jengo hilo litakuwa na ghorofa sita kwa ajili ya makazi ya watumishi wa umma.

“Mradi huu ni utekelezaji wa ila ya Chama Cha mapinduzi ya mwaka 2020 ambapo TBA tumeleekezwa kujenga nyumba za watumishi zenye uwezo wa kuchukua familia nyingi “amesema Urio.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela Kiomoni Kibamba amesema kuwa kuna uhaba wa nyumba za watumishi wilayani Ilemela.

hapo.

6 comments

Comments are closed.