Kata tano kunufaika na mradi wa skimu ya umwagiliaji wa sh bilioni sita

TANGA,Korogwe,Jumla ya kata tano zilizopo wilayani Korogwe zinakwenda kunufaika na fursa ya kilimo cha umwagiliaji kupitia utekelezaji wa Mradi wa skimu ya bonde la mto mkomazi wenye thamani ya sh Bilioni sita.

Mradi huo ambao unatekelezwa na serikali utaweza kuwanufaisha wakulima ambao wanalima mazao mbalimbali ikiwemo mpunga,mahindi pamoja na mazao ya mboga mboga.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji Manga Mkuu wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwegelo amesema kuwa kukamilika Kwa mradi huo kuna kwenda kutoa uhakika wa chakula Kwa wilaya hiyo na mkoa Kwa ujumla.

Advertisement

“Kwa mradi tunakwenda kumuhakikishia Rais Samia Suluhu kwamba Korogwe tutakuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha ziada ambacho kitaweza kutosheleza mkoa mzima na akiba kubaki”amesema DC Mwegelo.

Nae Mhandisi wa umwagiliaji mkoa wa Tanga Mhandisi Emmanuel Challo amesema  mradi huo unatarajiwa kuanza utekelezaji wake mapema mwezi ujao baada ya kukamilika Kwa upembuzi yakinifu.

Kata za Mkumbara,Mombo,Magila gereza,Mazinde na Chekelei zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe ndio ambazo zitaweza kunufaika na mradi huo wa umwagiliaji.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *