Katavi kujitegemea maonesho ya Nanenane 2024

KATAVI: Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Onesmo Buswelu ameagiza kuundwa kwa kamati maalumu itakayoratibu mchakato wa maandalizi ya sherehe za maonesho ya wakulima (nane nane) kwa mwaka 2024 ndani ya siku 10.

Ametoa maagizo hayo katika kikao cha maendeleo ya Wilaya ya Tanganyika kilichofanyika katika ukumbi wa Mkurugenzi wilayani humo ambapo kwa miaka mingi Mkoa wa Katavi umekuwa ukisafirisha wakulima kwenda kushiriki maonesho ya nane nane katika Mkoa wa Mbeya hali ambayo Buswelu ameeleza imekuwa ikiigharimu serikali fedha nyingi.

DC Buswelu amesema hali hiyo ilikuwa ikiwanyima fursa wakulima wengine kunufaika na sherehe hizo.

Kwa mujibu wa Afisa kilimo wa Wilaya ya Tanganyika Philemoni Mwita amesema maonesho hayo yatasaidia kuwafikia wakulima wengi zaidi katika Wilaya ya Tanganyika na Mkoa wa Katavi badala ya kutegemea maonesho ya kikanda yanayofanyika mkoani Mbeya.

Habari Zifananazo

Back to top button