Katibu tawala Arusha awapongeza walioacha uraibu

KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha, Mussa Misaile amewapongeza wanawake na wasichana waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya  ambao wamejitambua na kutoka kwenye maisha hayo ya kutumia dawa za kulevya .

Pongezi hizo  zimetolewa jijini Arusha alipofungua Kongamano la Wanawake na Wasichana 2025; lenye kauli mbiu ‘Tukatae Dawa za Kulevya’  sanjari na kuwakabidhi vifaa vya mama lishe ili wakaanzishe vijiwe vya kupikia na kuuza vyakula kwa watu mbalimbali.

Amesema wanawake ni nguzo ya taifa hivyo kuwapoteza kwa kuwaacha kwenye matumizi ya dawa za kulevya ni athari kubwa kwa kuwa wao ni nguvu kazi katika shughuli za uchumi hivyo akalitaka Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kuendelea na kudhibiti  matumizi ya dawa hizo.

Misaile amesema zipo changamoto mbalimbali za dawa za kulevya na zinahitajika nguvu ya pamoja  katika kupambana hivyo DCEA imeanzisha vilabu vya kupambana na dawa za kulevya kwenye shule na vyuo lengo ni kutoa elimu ya madhara ya matumizi ya dawa hizo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button