Kaze: Mechi kubwa inaamuliwa na wakubwa

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema mechi kubwa inaamuliwa na wachezaji wakubwa kama aliokuwa nao kwenye kikosi chake hivyo mchezo wa kesho dhidi ya Simba wamejipanga kucheza kitimu na kupata matokeo ya ushindi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kocha huyo amesema siyo kushinda lakini wamejipanga kuonesha kiwango bora ili kuwafurahisha mashabiki zaidi ya elfu 50 watakaohudhuria mchezo huo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Wachezaji wetu wote wapo sawa tumejiandaa kwa kila kona tunatambua utakuwa mchezo mkubwa Simba wana timu nzuri wanawachezaji mmoja mmoja wasumbufu hasa eneo la ushambuliaji lakini sisi tupo kitimu zaidi na tutalionesha hilo kesho,”amesema Kaze

Kocha huyo amesema furaha yao ni kuifunga Simba na kutangaza ubingwa mbele ya timu kubwa ambayo ni wapinzani wao wakubwa kwenye soka la Tanzani

Habari Zifananazo

Back to top button