Kazini kwa Vital’O kuna kazi leo
KLABU ya Vital’O ya Burundi ina kazi kubwa kupindua meza leo katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja Azam Complex, Dar es Salaam.
SOMA: Yanga yaipania Vital O mchezo wa marudiano CAF
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Agosti 17 kwenye uwanja huo huo Yanga ilishinda kwa mabao 4-0.
Kabla ya mchezo huo wa kwanza Vital’O iliitisha Yanga kwamba ingeisambaratisha vibaya.
Timu nyingine mbili za Tanzania zitashuka viwanja tofauti leo katika michezo ya marudiano.
Azam baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 kwenye wa Azam Complex itakuwa ugenini mjini Kigali kwenye uwanja Amahoro kuikabili APR.
Nayo JKU ya Zanzibar baada kukung’utwa mabao 6-0 na Pyramids itajiuliza leo iwapo itapindua meza au la kwenye uwanja wa The 30 June uliopo mji kuu wa Misri, Cairo.