Kelvin John aitwa Taifa Stars

KOCHA Mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars) Miguel Gamondi ameita kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwezi huu.

Kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 kujiwinda dhidi ya Kuwait katika mchezo utakaofanyika Novemba 14 uwanja wa Al Salam katika mji mkuu wa Misri, Cairo

SOMA: Klabu zisaidie kuzalisha wachezaji bora Taifa Stars

Gamondi amewataja wachezaji hao kuwa ni Yakoub Suleiman, Hussein Masalanga, Zuberi Foba, Bakari Mwamnyeto, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Alphonce Mabula, Mudathir Yahya, Wilson Nangu na Novatus Dismas.

Wengine Pascal Msindo, Ibrahim Abdulla, Haji Mnoga, Dickson Job, Habibu Idd, Tarryn Allarakhia, Charles M’mombwa, Suleiman Mwalimu, Feisal Salum, Morice Abraham, Abdul Suleiman, Paul Peter na Kelvin John.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button