WACHIMBA dhahabu wa Chunya mkoani Mbeya, Ken Gold leo imepata ushindi wa kwanza tangu kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuwachapa maafande wa JKT Tanzania kwa bao 1-0.
SOMA: Ken Gold yachekelea pointi ya kwanza Ligi Kuu
Bao hilo pekee la mchezo wa awali wa Ligi Kuu leo uliofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya limefungwa na Hebert Lukindo katika dakika 68.
Ken Gold imepoteza michezo 5 ya kwanza ya ligi hiyo na imetoka sare mchezo mmoja.
Michezo mingine inayofanyika leo ni kati ya Simba na Coastal Union unaopigwa muda huu kwenye uwanja wa KMC Dar es Salaam wakati Mashujaa inakabiliana na Singida Black Stars kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.