Ken Gold yachekelea pointi ya kwanza Ligi Kuu
KLABU ya Ken Gold imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Tabora United kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hivyo kupata pointi ya kwanza tangu kuanza msimu wa 2024/2025.
Kabla ya sare hiyo Ken Gold ilikuwa imepoteza michezo yake mitano mfulilizo.
SOMA: Ken Gold mikononi mwa Yanga Ligi Kuu leo
Ken Gold ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Herbert Lukindo katika dakika 12 kabla ya Tabora United kusawazisha kupitia Andy Bikoko dakika 77.
Michezo mitano Ken Gold iliyopoteza ni kama ifuatavyo:
Ken Gold 0-1 Yanga
Kagur Sugar 2-0 Ken Gold
KMC 1-0 Ken Gold
Fountain FG 2-0 Ken old
Ken Gold 1-3 Singida lack Stars
Mchezo wa Ken Gold wa Ligi Kuu unaofuata utakuwa dhidi ya JKT Tanzania Oktoba 4 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.