Ken Gold mikononi mwa Yanga Ligi Kuu leo

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo inashuka dimba la Sokoine jijini Mbeya dhidi ya Ken Gold iliyopoteza michezo yake yote ya ligi hadi sasa.

SOMA: Ken Gold waamua kuja kivingine

Yanga ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 3 baada ya mchezo mmoja wakati Ken Gold ipo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo haina ponti baada ya michezo 4.

Katika mchezo mwingine wa ligi leo Coastal Union itakuwa mgeni wa JKT Tanzania kwenye uwanja wa Major General Isamuhyo , Dar es Salaam.

JKT Tanzania ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 3 baada ya michezo 3 wakati Coastal Union inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 4.

Habari Zifananazo

Back to top button