Kenya yajipanga kutumia chanjo kwa mifugo

KENYA : RAIS William Ruto amewakejeli wanaopinga mpango wa chanjo ya mifugo uliopangwa kuanza Januari, 2025.

Rais Ruto amesema kuwa mpango huo utaimarisha wakulima ili kuendana na viwango vya kimataifa wakati wa kuuza bidhaa za nyama na ngozi nje ya nchi.

“Chanjo inatolewa kwa binadamu na sio hatari kuwachanja watu kwa nini iwe hatari kuwachanja wanyama?”, William Ruto ameuliza.

Advertisement

Hata hivyo, baadhi ya wafugaji nchini humo wanapinga matumizi ya chanjo kwa wanyama huku wakidai hawakupewa taarifa mapema. SOMA: Bil 460/- kuboresha sekta ya mifugo

Chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa ng’ombe milioni 20 dhidi ya Ugonjwa wa Miguu na Midomo na kondoo na mbuzi milioni 50 kote nchini Kenya.