Kerem Aktürkoğlu anasa rada za Man United

Winga wa Benfica, Kerem Aktürkoğlu.

TETESI za usajili zinasema Manchester United inalenga kumsajili wachezaji wawili wa Benfica, Kerem Aktürkoğlu na Orkun Kökçü lakini dili lolote lile huenda likagharimu euro milioni 70. Pia Tottenham Hotspur ina nia kuwasajili. (Caught Offside)

Arsenal na Manchester City ni miongoni mwa timu zinazoonesha nia kumsajili kiungo wa Atalanta, Charles de Ketelaere. (Caught Offside)

Kocha wa Brentford, Thomas Frank anafikiriwa ndiye anaongoza mbio kuchukua mikoba Manchester United. (Mail)

Advertisement

SOMA; Arsenal yaingilia usajili wa Nico Williams

Makocha wawili wanaopewa kipaumbele kuchukua mikoba ya Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City iwapo ataondoka ni Kocha wa Sporting CP, Ruben Amorim na Xabi Alonso wa Bayer Leverkusen. (Mail)

Barcelona inaonesha nia kuwasajili Jonathan Tah, Alphonso Davies na Jonathan David ambao watakuwa wachezaji huru majira yajayo ya kiangazi. (Mundo Deportivo

Real Madrid ingependa kumsajili kiungo wa Manchester City, Rodri, ingawa City iliyotwaa taji la Ligi Kuu England mara nane inaweza kumpa mkataba mpya. (GIVEMESPORT)