Kesi waliosababisha hasara Soko Kariakoo kusikilizwa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 20, mwaka huu, kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya kuingilia miundombinu ya umeme katika Soko la Kariakoo inayowakabili mfanyabiashara, Erick Rushenzirane na wenzake wawili.

Hayo yalijiri mahakamani hapo juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, kesi hiyo ilipotajwa ambapo Wakili wa Serikali, Caroline Matemu alieleza kuwa ushahidi wa kesi hiyo ulishakamilika na tayari washtakiwa walishasomewa maelezo ya awali.

Hata hivyo, wakili huyo alidai kuwa kesi ilishindwa kuendelea kwa sababu hakimu wa kesi hiyo, Mary Mrio ana jukumu la kusikiliza shauri la mauaji nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo.  Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Emmanuel Daroshi na Baruani Baruani wote wakazi wa Dar es Salaam.

Katika shauri hilo, washtakiwa  walidaiwa kuisababishia hasara ya zaidi ya Sh milioni 316 Mamlaka ya Soko la Kariakoo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa Januari 14, 2020 katika Soko la Kariakoo, washitakiwa hao kwa pamoja waliharibu miundombinu ya Tanesco kwa kukata nyaya za umeme zinazounganishwa kwenye transfoma na kuondoa baadhi ya vitu kwenye swichi ya transfoma jambo lililoisababishia Mamlaka ya Soko la Kariakoo hasara ya Sh milioni 316.9.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x