Kesi ya kujihusisha nyara za serikali yaahirishwa

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kujihusisha na nyara za serikali inayowakabili raia 11 wa Tanzania, umeomba kuahirisha kusikiliza kesi hiyo, baada ya baadhi ya mawakili kutokuwepo mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Tumaini Maingu, ameema hay oleo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rhoda Ngimilanga.

Maingu alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo, hivyo  aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kuanza kusikilizwa.

Hakimu Ngimilanga aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 9, mwaka huu na washitakiwa wataendelea kubaki rumande.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Victor Mawala, Haruni Abdallah, Abbas Hassan, Solomoni Mtenya, Khalfani Kahengele, Ismail Kassa, Juma Buguma, Kassim Saidi, Peter Nyachiwa, John Buhanza na Mussa Abdallah wote wakazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, inadaiwa  kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na nyara za serikali bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, ambazo ni vipande 660 vya meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.6.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa na mtandao mkubwa wa uhalifu wa ujangili, ambao unajihusisha na kuuza na kununua, kupokea na kuhamisha, kusafirisha nyara za serikaki ambazo ni meno ya tembo.

Habari Zifananazo

Back to top button