Khamenei bado anapata nafuu, aendelea kuongoza maamuzi

TEHRAN — Kiongozi Mkuu mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei, anaendelea kupata nafuu baada ya kujeruhiwa vibaya usoni na miguuni, lakini bado anashiriki kikamilifu katika maamuzi makubwa ya kitaifa, vyanzo vimeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Khamenei, mwenye umri wa miaka 56, hajaonekana hadharani tangu mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel mwanzoni mwa vita yaliyomuua baba yake, Ali Khamenei, pamoja na baadhi ya wanafamilia wake.

Vyanzo vilisema alipata majeraha makubwa yaliyosababisha ulemavu wa uso na kujeruhi miguu, ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi na serikali ya Iran.

Hata hivyo, vyanzo vya Marekani, vikiwemo maafisa wa ulinzi, vimeeleza kuwa Khamenei alijeruhiwa vibaya na huenda alipoteza mguu mmoja. Hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa na CIA.

Licha ya hali yake kiafya, taarifa zinaeleza kuwa Mojtaba Khamenei anaendelea kushiriki katika maamuzi muhimu, ikiwemo mazungumzo ya sitisho la vita na Marekani.

Wataalamu wanasema kiongozi huyo anatarajiwa kuendeleza msimamo mkali wa mtangulizi wake, hasa kutokana na uhusiano wake wa karibu na Islamic Revolutionary Guard Corps, taasisi yenye ushawishi mkubwa kisiasa na kijeshi nchini humo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button