JESHI la Polisi limesema limempata mtoto wa mwezi mmoja aliyeripotiwa kuibwa mapema mwezi huu huko Kagera na kwamba linawashikilia watu watano kwa tuhuma za wizi huo.
Mama wa Mtoto alilipoti Polisi Disemba 2 kuwa kichanga chake kimepotea katika mazingira ya kutatanisha na Jeshi lilianzisha operesheni maalumu iliyofanikisha kukipata kichanga hicho.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapo William Mwampaghale amesema watuhumiwa walimchukua mtoto huyo na kisha kumpeleka kwa mganga wa jadi katika kata ya Kamachumu wilayani Muleba ili mama wa mtoto asiwatafute.
“Baada ya kukamilisha hilo walitawanyika. Mtuhumiwa mmoja alipanda gari kuelekea Dar es Salaam akiwa na mtoto huyo. Alikuwa amepanga kwenda kuishi naye kama mwanaye hata hivyo alikamatwa akiwa mkoani Dodoma,” amesema Kamanda Mwampaghale
I don’t think the title of your article matches the content lol. Just kidding, mainly because I had some doubts after reading the article.