Kidata: Kampuni acheni biashara za magendo

DAR ES SALAAM: KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, Alphayo Kidata ameyataka makampuni na wafanyabiashara wakubwa kuepuka kufanya magendo kwa kuingiza bidhaa kinyemela na badala yake kufuata taratibu za uingizaji bidhaa ili kuliingizia taifa pato kwa kulipa kodi.

Amesema hayo katika sherehe ya mwendelezo wa utoaji tuzo kwa walipakodi bora kwa mwaka 2022/2023 jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, Serikali ya awamu sita imeendelea kufungua nchi hivyo ni vyema wafanyabiashara wakatumia wasaa huo kulipa kodi kwa wakati katika kuunga jitihada za serikali kukuza uchumi.

Katika hatua nyingine Kidata amesema TRA ilisimamia vizuri zoezi la ukusanyaji mapato nchini katika amalengo waliyowekewa mwaka 2022/23 ambayo wameyafikia kwa asilimia 97.4 kwani walikusanya Sh trilioni 24.11 kati ya Sh trilioni 24.76 walizopangiwa na kueleza kuwa hiyo si hatua ndogo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa huduma za mamlaka TCAA ambao ni miongoni waliopata tuzo, Teophory Mbilinyi amesema tuzo hiyo inatija kubwa katika mamlaka ya anga katika utendaji wao.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button