Kihenzile Cup: Vijana kazi kwenu
MBUNGE wa Jimbo la Mufundi Kusini na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile kwa kushirikiana na Taasisi ya Kihenzile Foundations amezindua Ligi ya Kihenzile Cup yenye lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika michezo sambamba na kutoa elimu ya kupiga kura kwenye chaguzi mbalimbali zinazokuja
Ligi hiyo ambayo inatarajiwa kushirikisha timu 16 zilizopo kwenye kata 16 za jimbo hilo itadumu kwa miezi mitatu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo, Naibu Waziri Kihenzile amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki katika ligi hiyo Ili kujenga afya zao lakini na kuweza kuibua vipaji vya wachezaji wa mchezo huo.
SOMA: Kihenzile akabidhi vifaa tiba vya Sh bilioni 1.8 hospitali
“Licha ya michezo kutumika kama sehemu ya kujenga afya lakini tutatumia fursa hiyo kuweza kutoa elimu ya mpiga kura Kwa wananchi mbalimbali ambao wataweza kufika kuangalia ligi hiyo Ili kuongeza uwelewa Kwa wananchi kuweza kushiriki kwenye chaguzi zinazokuja Kwa ukamilifu,”amesema Kihenzile.
Aidha ametaja zawadi kwawashindi mbalimbali wa ligi hiyo kuwa ni mshindi ngazi ya kata atapata Sh 500,000 ,seti Moja ya jezi nampira,mahindi wa pili atapata Sh 200,000 na seti moja ya jezi huku mshindi wa tatu atapata Sh 100,000 pamoja nampira huku zawadi ya mshindi ngazi ya Jimbo itatangazwa baadae.