Kihongosi awasili Manyara ziara ya kikazi

MANYARA: KATIBU wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi leo Juni Mosi,2026 amewasili katika Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ya Kikazi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Mkoa wa Manyara ni mkoa wa 11 Kihongosi kutembelea katika ziara zake za kukagua uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Baada ya kuwasili mkoani humo Kihongosi ameanza rasmi ziara yake katika Wilaya ya Hanang’ , kwa kuanza kupokelewa katika Kata ya Masakta na kuhudhuria kikao katika Shina Namba Moja Tawi la Masakta, anatarajiwa kukagua jengo la utawala la Halmashauri , Kukagua mradi wa Chujio la maji safi Kata ya Jorodom.

Pia Kihongosi anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Katesh kwa ajili ya kuzungumza, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button