Kihongosi: Msibebe ajenda, msitumike

MWANZA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi amewataka wananchi kutokubali kutumika vibaya kwa kubeba ajenda za watu wasizozijua.

Kihongosi ameeleza hayo leo Machi 10,2026 alipohudhuria kikao cha Shina namba mbili Tawi la Mashineni Kata ya Itumbili Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa zoara yake ya kikazo katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza baada ya kusikiliza ajenda ya kikao hicho Kihongosi amesema Tanzania ni ya kila mmoja, hivyo ni lazima ilindee, iheshimiwe na kuthaminiwa kama ambavyo ilijengewa misingi imara ya taifa lenye amani na utulivu.

Pia Kihongosi amesema kuwa watu hawapaswi kujenga chuki akiwataka wannachi kuelewa kuwa watu wa vyama tofauti wanaweza kushirikiana, kula pamoja na hata kuoana, hivyo amewataka wafanya siasa za kistaarabu bila kugombana kwa sababu ya vyama vya siasa, dini wala ukabila.

“Kama vyama vya siasa vinaojenga chuki hazina mantiki Chadema wanamchukia CCM, CCM wanawachukia CUF , CUF wanawachukia Chauma, Chauma anakukiya Shuwata huo ni ushamba wa kisiasa. Siasa ya kweli, watu wanashikamana, wanapendana, wanakula pamoja na wanaowana wa vyama tofauti,” amesema kihongosi.

Ameongeza watu wanapaswa kufanya siasa za kistaarabu badala ya kugombana kwa sababu ya vyama vya siasa, dini, ukabili au ukanda, kwani ili wajenge taifa moja lazima kudumisha umoja wao.

Pia Kihongosi amesema kupitia migogoro ya kisiasa ni wazi wnaaoumia ninwannachi w akawaida na si viongozi wa juu, hivyo amewataka watu waukemee ushabiki wa kisiasa, na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kujipatia riziki na washikamane na kufanya mazungumzo.

“Shikamaneni hapo wewe ukifa leo hutazikwa na chama cha siasa, utazikwa na watanzania hawa wamazungumzo. Hawa ndiyo watachimba kaburi lako, watabeba jeneza lako na hawa ndiyo watakuweka chini ya ardhi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button