Kihongosi: Tunzeni miradi ya maendeleo

SHINYANGA: KATIBU Wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amewataka wananchi kutunza miundombinu na miradi ya maendeleo inayojengwa kwani ni urithi wao.

Kihongosi ameeleza hayo leo Machi 5,2026 alitembelea katika mradi wa ujenzi wa daraja la Ubagwe lililopo katika barabara ya mto Mwabomba-Igombe yenye urefu wa mita 60 katika Halmashauri wa Ushetu wikayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Kihongosi alisema CCM itaendeke kuwapelekea huduma bora kwa wananchi wake, akiwaomba waendelee kuwa na imani nao.

“Tangu kupatikane kwa uhuru daraja hili halijawahi kujengwa lakini lilijengwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwanamama hodari, madhubuti na mchapakazi na mwenye upendo,” alisema Kihongosi.



