KIKOSI cha timu ya taifa “Taifa Stars” kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN) 2024 dhidi ya Sudan kimetangazwa.
Kikosi hicho cha wachezaji 24 kinaundwa na vijana zaidi.
Wachezaji walioitwa watakaokuwa chini ya Kocha Bakari Shime ni Aisha Manula, Isaya Kissanga, Antony Mpemba, Pascal Msindo, David Braison, Nickson Mosha, Lameck Lawi, Abdulrahim Bausi, Vedastus Masinde na Ibrahim Ame.
SOMA: Kila la heri Taifa Stars
Wengine ni Hijjah Shamte, Adolf Mtasingwa, Abdulkarim Kiswanya, Charles Semfuko, Shekhani Hamis, Ahmed Pipino, Sabri Kondo, Salum Ramadhan, Ismail Kader, Bakari Msimu, William Edgar, Seleman Mwalimu, Valentino Mashaka na Cyprian Ngushi.