Kikwete ahitimisha ziara yake Bukina Faso

UJUMBE Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amehitimisha ziara yake kwa kukutana na Rais wa Burkina Faso, Captain Ibrahim Traoré.

Akizungumza na Rais Traore, Kikwete aliwasilisha ujumbe maalum na salamu za Rais Samia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika, hususan kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja Afrika iweze kuendeleza rasilimali zake kwa faida ya watu wa bara lao.

“Rais wangu amenituma nije kuwasilisha Ujumbe Maalum kwako na nimefurahi umenipa fursa hiyo na leo umeupokea rasmi”, Alisema Kikwete. Mkutano huo ulifanyika jijini Ouagadougou, Burkina Faso Aprili 17, 2025 na kuhudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka Serikali zote mbili.

Katika mazungumzo yao Kikwete alielezea shukrani zake kwa kupata fursa ya kukutana na Captain Traoré.

 

Habari Zifananazo

Back to top button