Kila kaya kulima kahawa Missenyi

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi bajeti ya Sh milioni 150 kwa mwaka 2025/2026 kutoka bajeti ilikuwepo awali ya Sh milioni 130 kwa ajili ya wananchi wote kujihusisha na kilimo cha kahawa ili kukidhi maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha Tanzania inaongeza uzalishaji wa kahawa kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 25 ifikapo mwaka 2030.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, ProjestusTegamaisho aliongoza majadiliano ya kuweka mikakati ya pamoja kuinua kilimo cha kahawa wilayani humo na madiwani  wa halmashauri hiyo kwa pamoja wanakuwa msitari wa mbele kuhakikisha wananchi wao wanalima  kahawa kama zao mkombozi wa wananchi.

Amesema kuwa baraza hilo linawataka wanachi  wa Missenyi kila kaya kuwa na miche ya kahawa angalau 20 hadi 30 huku akimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuanza kutenga maeneo Kwa ajili ya vijana na wanawake walioko tayari  kulima kahawa kwa wingi.

“Tulivyokuwa katika mkutano wa nchi 25 zinazolisha kahawa tuliona mfano wa nchi ya Ethiopia ambao nchi yake inaendeshwa na uchumi wa kahawa na kama Rais wetu alivyosema anatamani kilimo kichangie asilimia 2 ya Bajeti ya Taifa ,sisi Missenyi kwa pamoja na Baraza hili tunaongoza ajenda na tuko tayari kwa mapambano kwa kuanza Kuna mbegu mpya ambayo  haijali kiangazi wala mvua niko tayari kugawa hata Miche mitatu kwa kaya zote za Missenyi, “alisema Tegamaisho

Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ofisa kilimo na mifugo Tapita Solomon amesema kuwa halmashauri hiyo sasa imedhamiria kugawa miche zaidi kwa  kugawa miche ya kahawa ni 1,200,000 kwa msimu huu ukilinganisha na miche ya awali iliyopangwa kugaiwa 717,228.

Alisema kuwa  kutokana na dhamira ya kila mmoja kutaka wananchi wainue uchumi wao kupitia kilimo cha kahawa na kufanya ajenda ya kulima kahawa kuwa ya kudumu kuanzia vijiji Hadi Wilaya  mwaka huu   imeweka mikakati wa kuhakikisha  Kila kaya inapaswa kuanza kuvuna  kahawa kilogram 300 hadi 1,000 kufikia mwaka 2030

Amesema halmashauri hiyo inapanga kuwashirikisha vijana zaidi na kuongeza idadi ya wanawake  katika uzalishaji wa kahawa kwa kuwapa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi hayo

“Tunaendelea kuweka mazingira bora ya mauzo ya kahawa ili kuendelea kuboresha bei ya kahawa ,pia tutaendelea kuhamasisha matumizi ya ndani ya kahawa ,kwa sababu bei ya sasa ya kahawa ni shilingi 6,000 na miaka muchache nyuma ilikuwa shilingi 1,000 hii ni hatua kubwa sana “alisema Solomon.

Kikao cha tatu cha nchi zinazolima kahawa barani Africa G25  kikifanyika February 21,22 mwaka huu  nchini Tanzania kikiwa na lengo la kufungua fursa za ajira kwa vijana na kufufua Mnyororo wa Thamani wa zao la kahawa barani Africa.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button