Kilimo kuwa chanzo kikubwa pato la taifa

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali inalenga kukifanya kilimo kuwa chanzo kikubwa cha kuchangia katika pato la taifa.

Akizungumza leo eneo la Litola Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma Rais Samia amesema kilimo kimekuwa sekta kubwa ya uzalishaji inayoiingizia serikali fedha kwa uharaka zaidi.

Rais Samia pia amewahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono katika sekta ya kilimo ikiwemo  kutoa ruzuku mbalimbali.

SOMA: Rais Samia apongezwa maono wizara ya kilimo

“Kwa sasa serikali inatoa ruzuku ya mbolea, lakini pia nimemuagiza waziri aweke ruzuku ya mbegu, bei za mbegu zitashuka, kwasababu serikali itabeba nusu ya gharama yake,”amesema Rais Samia.

Kiongozi huyo wa nchi ameonya uchomaji moto mashambani kwani vitendo hivyo vinaharibu mazingira na misitu iliyohifadhiwa.

Aidha, Rais Samia amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa bidii hasa katika sekta ya kilimo ili kuendelea kuchangia mapato.

Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Victor Kawawa ameipongeza na kuishuruku serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali wilayani humo, iliyotatua changamoto za wananchi ikiwemo upatikanai wa maji na barabara zinazopitika.

Habari Zifananazo

Back to top button