Rais Samia apongezwa maono wizara ya kilimo
KITENDO cha Rais Samia Suluhu Hassan kutenga bajeti kupitia Wizara ya Kilimo na kufanya mageuzi kwenye sekta hiyo kwa kuwawezesha wakulima kufanya kilimo chenye tija, kimemvutia Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye hivyo kumshukuru kiongozi huyo wa nchi kwa maono yake hayo.
Akizungumza leo Agosti 21 wakati wa kukabidhi vitendea kazi kwa maofisa ugani mkoani humo, RC Andengenye amesema nyenzo hizo zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na serikali katika kukifanya kilimo kuwa na tija kubwa.
SOMA: Vijana watakiwa kuchangamkia fursa kilimo
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wakati huu ambao serikali inautangaza mkoa huo kuwa wa kimkakati katika masuala ya uchumi na biashara sekta hiyo ina umuhimu mkubwa katika kutekeleza mpango huo kwani sekta hiyo inagusa maisha wananchi wote.
Alisema kuwa asilimia 70 ya wakazi wa Kigoma hutegemea shughuli za kilimo kama chanzo chao kikuu cha uchumi kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku hivyo ametaka nyenzo hizo zilizokabidhi zitumike katika kutekeleza mikakati ya kuimarisha shughuli za kilimo na kuwafikia wadau wote wa kilimo kwa wakati