Wiki ya ACT Wazalendo kutamatika Kilwa Mei 5

DAR ES SALAAM: CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kitaadhimisha wiki ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa chama hicho kuanzia Aprili 29, 2026 na kuhitimishwa Mei 5, 2026 katika Jimbo la Kilwa Kusini, mkoani Lindi.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 27, na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Shangwe Ayo imeeleza kuwa hatua hiyo ni utaratibu na utamaduni wa chama hicho kukumbuka na kuadhimisha kuzaliwa kwake.

“Shughuli mbalimbali za kijamii na kisiasa zitafanyika katika mikoa yote nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo na kitaifa shughuli za maadhimisho zitafanyika katika jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi,” ameeleza Shangwe Ayo.

Ameeleza kuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ‘Ukweli, Haki na Uwajibikaji Msingi wa Maridhiano’.

“Katika kusimamia masuala haya, Chama kitatuma ujumbe wa mshikamano kwa wananchi na wapenda mabadiliko kote nchini, na kwamba ACT Wazalendo kitakuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kudai misingi hiyo”.

Tunatoa wito kwa wapenda haki, demokrasia na mabadiliko kote nchini kuungana pamoja na ACT Wazalendo katika dhamira na adhima yetu hii tunapokwenda kuadhimisha miaka 12 tangu kuzaliwa kwa chama chetu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button