Kinana aipongeza China ujenzi VETA Kagera

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, ameipongeza Serikali ya China kwa kufanikisha ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ambao umegharimu Sh.  Bilioni 22.

Kinana ametoa pongezi hizo mara baada ya  kukagua hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa chuo hicho, kilichopo mkoani Kagera.

Kinana amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Jamhuri ya Watu wa China, zimekuwa kwenye uhusiano wa Kirafiki wa muda mrefu, ambao ulidumishwa kutoka kwa waasisi wa mataifa hayo mawili.

“Nataka nichukue nafasi hii kuipongeza serikali kwa kazi nzuri inayofanya chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika sekta zote, ninyi ni mashahidi tangu Rais ameingia madarakani shule nyingi zimejengwa, vyuo vingi vimejengwa na walimu wameajiriwa na wanafunzi wameongezeka.

“Nina hakika Watanzania wengi wataelimika, kwa hiyo nampongeza Rais kwa kazi nzuri anayofanya, nichukue nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Jamhuri ya Watu wa China, niishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China , niseme bila kusita tunao marafiki wengi, ” ameeleza Kinana.

Katika hatua nyingine Kinana amekutana na kuzungumza na wana CCM Mkoa wa Kagera, ambapo pamoja na mambo mengine amewakumbusha viongozi kuwajibika na kuwatumikia wananchi pamoja na kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.

Habari Zifananazo

Back to top button