Kinana ampigia chapuo Rais Samia

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahaman Kinana, amesema 2025 njia itakua nyeupe kwa  chama hicho kushika Dola kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa ndani ya miaka miwili ya uongozi wake.
Kinana, ameyasema hayo leo Julai 23, 2014 katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Dk.

Ashatu Kijaji kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2023.

pharmacy

Amesema, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amepata mafanikio makubwa ndani ya miaka miwili ya uongozi wake kutokana  na utulivu, usikivu, kupokea ushauri na kufanya uamuzi wa busara kwa manufaa ya Watanzania.
“Kwa hali ilivyo na kwa hatua tuliyopiga tukienda hivi tunavyokwenda mpaka kufika 2025 nina uhakika kila Mtanzania atakuwa na sababu ya kusema tuendelee na CCM, tuendelee na Rais Samia Suluhu Hassan.” Amesema na kuongeza
” Hatutakua  na sababu nyingine yoyote kwanza ni utamaduni wetu Chama Cha Mapinduzi hatubadilishi uongozi katikati ya safari, ukitaka kubadilisha sababu itakuwa nini, hakuna.
“Hatusemi haya kwa kujivuna bali kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM lakini tunaangalia na wenzetu wa nchi jirani wanakwendaje.”Amesema
Kinana, amesema nchi  imetulia, ina amani, ina umoja, inamshikamano, nchi ina malengo, na ina mipango ambayo inatekelezwa na kila mtu ni shahidi, CCM itaendelea kuchaguliwa kwa sababu ina sera nzuri ina ilani nzuri inayotekelezeka.
Aidha, ameema kutokana misingi imara iliyowekwa na waasisi wa Taifa,  watu waliojaribu kuigawa nchi kwa misingi ya udini wameshindwa.
“Kuna watu wamejaribu kutugawa kwa misingi ya ukabila wameshindwa, kuna watu wamejaribu kutugawa kwa misingi ya ubara na visiwani wameshindwa,” amesema.
Advertisement

3 comments

Comments are closed.