Bobi Wine kufanyiwa upasuaji
UGANDA : KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu Bobi Wine amepangwa kufanyiwa upasuaji baada ya kudaiwa kupigwa risasi na askari polisi.
Taarifa zinasema Bobi Wine atafanyiwa upasuaji baadaa ya kujeruhiwa mguu katika tukio la vurugu lilitokea mjini Kampala.
Wakili wa Mwanasiasa huyo, George Musisi amesema Bobi Wine hayuko katika hali mbaya ingawa madaktari wamemfanyia upasuaji ili waweze kuondoa vipande vya risasi katika miguu yake.
Hapo jana Bobi Wine alikimbizwa katika hospitali ya Nsambya akiwa katika maumivu makali.
Jeshi la polisi nchini Uganda limepanga kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.