Kipa Mlandizi Queens atua Yanga Princess
KLABU ya mpira wa miguu kwa wanawake, Yanga Princess imemtambulisha golikipa mpya, Ester Kolonely kutoka timu ya Mlandizi Queens ambaye amekwenda kuongeza ushindani kwenye kikosi hicho.
Klabu hiyo imemtambulisha golikipa huyo leo ikisema tayari ameanza majukumu yake akiungana na wenzake katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.
SOMA: Yanga Princess kulipa kisasi Kariakoo dabi?
Ester alikuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia benchi la ufundi la Yanga Princess kwa umahiri wake wa kudaka na kupangua.

Yanga Princess imekuwa na mwendelezo wa kutambulisha usajili mpya wakiboresha kikosi chao ili kurejea kiushindani.
Tayari imewatambulisha wachezaji Wincate Kaari anayerejea kunako klabu hiyo akitokea Simba baada ya kujiunga nao msimu uliopita akitokea Yanga.

Wengine ni Riticcia Nabossa na Precious Christopher ambaye amerejea baada ya msimu uliopita kucheza Simba.



