KATA ya Kitangiri imeitandika kata Nyamanoro mabao 3-0 katika mchezo wa kundi A mashindano ya The Angeline Jimbo Cup uliopigwa leo uwanja wa Kona ya Bwiru wilayani Ilemele Mwanza.
Katika michezo mingine iliyochezwa leo kundi B Nyasaka imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Kiseke katika uwanja wa Sabasaba. Katika Kundi C,Nyakato ilitoka sare ya bila kufungana na Kahama katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari Buswelu.
Katika kundi D, Kayenze ilitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Bezi katika uwanja wa shule ya msingi Bugogwa.
Naye mratibu wa mashindano hayo Almas Moshi amewashukuru mashabiki na wadau wa soka kwa kuweza kujitokeza katika mashindano hayo.
Amewaomba mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo yanayochezwa katika viwanja vya kona ya Bwiru,shule ya msingi Sabasaba, shule ya msingi Bugogwa na shule ya sekondari Buswelu.
Comments are closed.