KITUO kikubwa cha mikutano kiitwacho Mount Kilimanjaro Convention Center kinatarajiwa kujengwa jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kituo kitakuwa na ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 3,000 2, eneo la maonesho lenye kuchukua watu 10,000, hoteli mbili za Nyota Tano zenye uwezo wa kulaza wageni 1,000.
–
Pia amesema kitakuwa na majengo ya nyumba za kuishi (apartments), kumbi ndogo za mikutano, majengo ya maduka (shopping malls), Nyumba za kulaza watu mashuhuri wakiwemo marais 8, maeneo ya kupumzika (recreation areas), maeneo ya burudani na bustani
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Ephraim Mafuru amesema uwekezaji huo ni mkubwa na utafungua fursa za kiuchumi kwa Mkoa wa Arusha.
–