Kivumbi Barca vs Inter Ulaya leo
NYASI za uwanja wa Olimpico Lluis Companys jijini Barcelona, Hispania leo zitawaka moto wakati wenyeji klabu ya Barcelona itakapoikaribisha Inter Milan ya Italia katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya(UCL).
Pilato wa mechi hiyo ni mwamuzi Clement Turpin wa Ufaransa.
SOMA: Arsenal vs PSG: Kibabe Ligi ya Mabingwa Ulaya
Kutinga hatua hiyo, Barcelona imeitoa Borussia Dortmund kwa jumla ya mabao 5-3 wakati Inter imeiondosha Bayern Munich kwa jumla ya mabao 4-3.
Kwa mara ya mwisho Barcelona na Inter zilikutana katika michuano hiyo msimu wa 2022/2023.
Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza iliyopigwa Aprili 29 kwenye uwanja wa Emirates jijini London, England wenyeji Arsenal imeshindwa kutamba mbele ya mashabiki wake baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Paris Saint-Germain.



