Kivumbi Ligi ya Mabingwa wanawake Ulaya

MICHEZO minne ya Ligi ya Mabingwa wanawake barani Ulaya inapigwa leo kwenye viwanja tofauti.

Mechi ya kibabe ni kati ya Chelsea na Real Madrid itakayopigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, London.

SOMA: Carneiro kurejea Chelsea?

Advertisement

Lyon ya Ufaransa itakuwa mwenyeji wa Galatasaray ya Uturuki kwenye uwanja wa Groupama Academy, uliopo jiji la Lyon.

Wolfsburg ya Ujerumani itakuwa mgeni wa Roma ya Italia kwenye uwanja wa Tre Fontane katika jiji la Rome.

Mchezo mwingine wa Ligi hiyo ya mabingwa Ulaya wanawake itahusisha Celtic kutoka Glasgow, Scotland dhidi ya FC Twente ya jiji la Enschede, Uholanzi.