NUSU fainali mbili za Ngao ya Jamii wanawake zinapigwa leo ikiwemo kati ya Simba Queens na Yanga Princess.
Mechi hizo zitafanyika kwenye uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
SOMA: Walete waletee! Simba Vs Yanga
Nusu fainali nyingine itazikutanisha JKT Queens na Ceasiaa Queens mechi itakayotangulia kwenye uwanja huo.
Michezo hiyo ni kiashiria cha ufunguzi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2024/2025.
Comments are closed.