Kivumbi tuzo za filamu 2023
DAR ES SALAAM: Bodi ya Filamu imetangaza rasmi washindi waliofanikiwa kuingia katika vinyang’anyiro mbalimbali vya tuzo za filamu mwaka 2023 zinazotarajiwa kufanyika December 16, 2023.
Akiongea na waandishi wa habari katibu mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Kiagho Kilonzo amesema tuzo za mwaka huu zipo tofauti na zilizopita kuanzia mchakato mpaka mfumo,
Amesema mwaka huu filamu zilizopita ni 57 na washiriki 59 kutoka Tanzania huku Afrika Mashariki ni filamu 30 tu.
“Mwaka huu majaji ndio watachagua nani anaefaa kwenye kipengele gani huku wapiga kura nao wakiwa na nafasi ya kupiga mpaka kwa simu ndogo.
‘amesema