TIMU ya KMC leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
SOMA: Mashujaa wazindukia kwa KMC
Mabao yote mawili ya KMC yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika za 16 na 60 wakati bao pekee la kufutia machozi la Tanzania Prisons limefungwa na Oscar Mwajanga katika dakika 74.