Kocha Mkwasa ajiuzulu Ruvu Shooting

Kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa ameikacha timu hiyo kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mkwasa amesema amefikia uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa watu wengine kuendeleza pale ambapo ameishia, huku akiiacha timu hiyo kwenye nafasi ya 15 ya msimamo ambayo ni ya pili kutoka mwisho.

“Labda falsafa yangu imeshindwa kufanya kazi, hivyo natoa fursa kwa mtu mwingine,” amesema Mkwasa.

Ruvu Shooting chini ya Mkwasa imecheza michezo 15 hadi sasa, ushindi mara tatu, sare mbili na wamepoteza michezo kumi ambayo ni mingi kulinganisha na timu yao ya msimu uliopita. Mechi inayofuata watamenyana dhidi ya Ihefu. 

 

Habari Zifananazo

Back to top button