DAR ES SALAAM; CHUO Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimeandaa Kongamano maalum la miaka 60 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1963.
Kongamano hilo linaenda sambamba na upimaji wa afya bure kwa wananchi ikiwemo magonjwa ya moyo, sukari, presha, na magonjwa ya saratani.
Akizungumza leo Novemba 13,2023 Kaimu Mkuu wa chuo cha MUHAS, Profesa Apolinary Kamuhabwa amesema, katika kuadhimisha miaka 60 ya MUHAS siku ya Alhamis wiki hii kutakua na kongamano la mada mbali mbali zitakazoelezea kilipotoka chuo hicho, kilipo na kinapokwenda.
“Wakati chuo kinaanza kilianza na wanafunzi 10 wa Diploma ya Utabibu, leo kila mwaka tuna wanafunzi zaidi ya 4,000 tunawatahini kila mwaka, “amesema.
Amesema, wakati chuo hicho kinaanzishwa kilianza na Programu moja na sasa walizonazo ni programu 101 na kati ya hizo programu 81 ni za uzamili na uzamivu.
Profesa Kamuhabwa amesema mgeni rasmi katika kongamano hilo ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.
Comments are closed.