Korea Kaskazini yafyatua kombola la balestiki usiku
KOREA Kaskazini imerusha kombora la balestiki katika Bahari ya Japan leo Jumatano, Julai 12 ikiwa ni saa kadhaa baada ya Pyongyang kuishutumu Marekani kwa kupeleka ndege za kijasusi katika eneo lake la kipekee la kiuchumi.
Wanadhimu Wakuu wa Jeshi la Pamoja (JSC) wa Korea Kusini wamesema tukio hilo pia lilithibitishwa na Tokyo.
Kombora hilo, ambalo lilirushwa mwendo wa saa 10 asubuhi kwa saa za huko, lilitarajiwa kuanguka baharini kilomita 550 mashariki mwa Peninsula ya Korea, Waziri wa Ulinzi wa Japan Yasukazu Hamada alisema, kama ilivyonukuliwa na Kyodo News.
Siku ya Jumatatu, Kim Yo-jong, Afisa Mkuu wa sera za kigeni wa Pyongyang na dada wa kiongozi wa kitaifa Kim Jong-un, aliahidi athari za “wazi na thabiti” dhidi ya Washington.
Makombora hayo yaliyoripotiwa baada ya Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wote kuondoka kuhudhuria mkutano wa NATO huko Vilnius, Lithuania. Viongozi hao watakutana kando ya hafla hiyo siku ya Jumatano.