Korosho, Jeshi Stars zaanza vyema Muungano Cup

KATIKA mwendelezo wa michuano ya wavu kuwania Kombe la Muungano inayoendelea kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), timu za Korosho Queens, Jeshi Stars na Mafunzo zimeanza vyema michuano hiyo.

Kwa upande wa wanawake, Korosho Queens waliibuka kidedea kwa kuwachapa KMKM seti 3-0 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Mafunzo nao hawakuwa na masihara, wakawazima Chui bila huruma kwa seti 3-0. JKT waliendeleza rekodi yao ya ushindi kwa kuwatoa Orkeeswa kwa ushindi wa moja kwa moja wa seti 3-0.

Katika upande wa wanaume, Jeshi Stars waliingia dimbani dhidi ya Moro Warriors na kuibuka na ushindi wa seti 3-1 katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki.

Timu ya High Voltage iliwalaza JKU seti 3-0, huku Nyuki wakifanya hivyo hivyo kwa wenyeji wa UDSM.

Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF), Shukuru Ally, amesema kuwa ushindani katika michuano hiyo unazidi kuongezeka kila siku.

Alitaja changamoto ya mvua kuwa kikwazo kikubwa katika ratiba ya michuano hiyo, kwani mechi nyingi zinachezwa kwenye viwanja vya wazi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button