Korosho kuuzwa kwa namba maalum ya mkulima

SERIKALI itaanza kuuza korosho kupitia namba maalum ya usajili ya mkulima ili kudhibiti changamoto ya utoroshaji pamoja na kuchepushe malipo ya mkulima katika msimu wa mauzo wa mwaka 2023/24 .

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa tasnia ya korosho msimu wa 2022/23 uliofanyika mkoani Tanga.

Amesema kuwa Kwa kufanya hivyo itasaidia serikali kupata mapato yake lakini na mkulima kuweza kunufaika na mauzo ya mazao yake.

“Tumejinga kuanzia mzimu huu korosho yote itakuwa kwa mfumo wa namba ya usajili ya mkulima ambayo aliitumia wakati wa kupata pembejeo lengo na kumsaidia mkulima lakini na serikali kupata takwimu sahihi ya uzalishaji wa zao hilo.”amesema Mavunde.

Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania, Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile amesema kuwa katika msimu wa mwaka 2022/23 jumla ya korosho ghafi zaidi ya tani milioni 176.6 ziliweza kukusanywa na kuingiza zaidi ya Sh bilioni 328.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button