Kortini akidaiwa kusafirisha dawa za kulevya

RAIA wa Marekani, Brandon Summerlind (30) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mescaline gramu 56.04.

Brandon alisomewa mashitaka jana na wakili wa serikali, Tumaini Maingu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

Tumaini aliieleza mahakama kuwa Novemba 12 mwaka jana katika Ofisi za Posta, Ilala katika Jiji la Dar es Salaam mshitakiwa alisafirisha gramu 56.04 za dawa ya kulevya aina ya Mescaline.

Advertisement

Tumaini alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama tarehe nyingine kwa ajili ya kusoma hoja za awali.

Tumaini aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa hatakiwi kupatiwa dhamana kwa mujibu wa sheria kwa kuwa anakabiliwa na kesi ambayo kiwango cha dawa kimezidi gramu 20.

Mshitakiwa amekana shitaka na kurudishwa rumande hadi Februari 7 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *