Kumekucha Chamazi fagio la chuma linaendelea kupita

MATAJIRI wa kusini mwa Dar es Salaam Azam Fc wameendelea na maboresho kwenye kikosi chao baada ya mapema leo kutangaza kuachana na makocha wawili wa timu hiyo kazi imeendelea huko chamazi.
Timu hiyo imetangaza pia kuachana na nyota wao Bruce Kangwa raia wa Zimbabwe aliyedumu kikosini hapo kwa misimu Saba ,Kangwa alikuwa nahodha wa timu hiyo alijiunga na Azam Fc mwaka 2016 akitokea Highlanders ya Zimbabwe.
Timu hiyo pia imeachana na kiungo wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna pamoja na Mshambuliaji kutoka Zambia Rodgers Kola.
Azam imepania kufanya maboresho makubwa kwenye timu hiyo kwani tayari ilishamtangaza kocha mpya kwa ajili ya msimu ujao lakini pia ilikamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Tanzania Feisal Salum