Kumekucha riadha Kanda ya Ziwa

ZAIDI ya wanariadha 1400 kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa na maeneo mbalimbali nchini wanatarajia kushiriki katika mashindano ya riadha ya ‘Transec Lake Victoria marathon’ kwa msimu wa tatu yatakayofanyika Julai 2, 2023 mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa mbio hizo. Halima Chake wakati wa uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa Mwanza Yatch club.

Chake amesema kutakuwa na mashindano ya kilomita 2.5 kwa watoto chini ya umri wa miaka 10, kilomita 5, kilomita 10 na kilomita 2.1

Amesema gharama za ushiriki kwa kiliomita ni Sh 20,000, kilomita 5 ni Sh 30,000, kilomita 10 ni Sh 35,000 na kilomita 21.1 ni Sh 35,000.

Amewashukuru wadau mbali mbali kwa udhamini wao katika mbizo zao ambapo baadhi ya wadau ni Transec, benki ya KCB,TBL na Konyagi.

Naye Katibu Tawala msaidizi wa Mkoa wa Mwanza upande wa uwekezaji na Biashara Patrick Karangwa ameushukuru uongozi wa Lake Victoria marathon kwa kuandaa mbio hizo.

Ameziomba kampuni na mashirika mbali mbali kujitokeza kwa wingi katika kuunga mkono mbio hizo.

Naye ofisa Mwakilishi wa kampuni ya Transec Victor  Okeyo amesema kamouni yao itaendlea kuchangia kwa kile kinachoweza kufanikisha lengo la kuisaidia jamii.

Amesema mbio ni sehemu mojawapo ya vitu vinavyotusaidia kuwa na afya bora. Alisema anawaomba wanamichezo washiriki kwa wingi katika mbio hizo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button