Kuna changamoto ya usalama Urusi-Uingereza

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema kuwa taifa la Urusi linakabiliwa na changamoto kubwa zaidi ya usalama kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni, kufuatia kile ilichokisema kuwa ni hatua ya vikosi vya Wagner Group kuelekea Moscow.

“Katika saa zijazo, uaminifu wa vikosi vya usalama vya Urusi, na haswa Walinzi wa Kitaifa wa Urusi, itakuwa muhimu kwa namna mzozo huu utakavyoisha. Hii inawakilisha changamoto kubwa zaidi kwa serikali ya Urusi katika siku za hivi karibuni,” wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema katika riporti ya kawaida ya kijasusi.

Advertisement
5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *