Kwa nini uanike faragha zako kwenye daladala?
UMEWAHI kushuhudia watu/mtu kwenye chombo cha usafiri wa umma iwe daladala, mwendokasi au hata magari mengine ya abiria akizungumza kwa sauti ya juu ama na mtu mwingine au kwa simu akianika mambo yake kwa kadamnasi?
Kama hujawahi, basi subiri ipo siku utashuhudia. Siyo tu kwenye vyombo vya usafiri, bali watu hao hushuhudiwa pia kwenye mikusanyiko mingine ya watu kama vile kanisani, sokoni au shuleni.
Watu wa aina hiyo hugeuka kikwazo kwa watu wengine kutokana na kuzungumza kwa sauti ya juu faragha zao kana kwamba wanahutubia.
Baadhi huzungumza mambo nyeti kuhusu ofisini, familia ikiwa ni pamoja na kujadili majina ya watu hadharani bila kujali waliowazunguka.
Huwa haiingii akilini kuona mtu ndani ya daladala anazungumzia watu wengine kwa kutaja majina yao, nyadhifa na ofisi zao bila kufikiri kwamba miongoni mwa kadamnasi inawezekana wamo ndugu, jamaa na marafiki.
Wengine hudiriki kuanika masuala ya fedha na biashara mbele ya watu bila kujali kuwa inaweza ikawa njia mojawapo ya kukaribisha huduma dhidi yao. Wakati mwingine, watu wa namna hiyo hugeuka kichekesho kwa kusema mambo ya uongo au kupotosha juu ya mambo wanayozungumza kwa sauti ya juu bila kufahamu kuwa wapo watu wanaofahamu sawia.
Pamoja na kwamba watu wa namna hiyo hawavunji sheria yoyote ikizingatiwa kwamba katiba inatoa uhuru wa kujieleza, lakini ipo haja ya kuelimishwa faida na hasara za upayukaji ama wakati wa kuzungumza kwenye simu au ana kwa ana na mtu mwingine.
Ifahamike upayukaji bila kuzingatia faragha yako au wengine si ustaarabu.
Lakini pia ni kitendo kinachoweza kuanika siri zako na za wengine na kuhatarisha usalama wako na mali zako.
Wapo baadhi ya watu waliojikuta mikononi mwa matapeli, wezi na wahalifu wengine kutokana na kuanika mambo yao kwa njia hiyo ya kuzungumza hovyo kwenye kadamnasi. Katika semina ya hivi karibuni kwa wanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi alikumbusha umuhimu wa kuwa na mipaka ya kuanika mambo binafsi.
Soma pia: Laini za simu milioni 72.5 zimesajiliwa
Mabel alihadharisha pia juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuanika taarifa nyeti, akisema kunatoa fursa kwa matapeli au wezi kutekeleza uhalifu kwa mhusika.
Wakichangia mada hiyo, baadhi ya washiriki walisema wapo watu wanaoponzwa na ushamba, uelewa mdogo au ulimbukeni kiasi cha kutuma picha na taarifa zao zote kwenye mitandao.
Ndiyo maana TCRA imeendelea kuelimisha jamii juu ya suala zima la faragha hususani upande wa mawasiliano kwa simu za mkononi.
Katika kitabu chake cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, TCRA inasisitiza watumiaji wa simu kuzingatia faragha yao na watu wengine.
“Chukua tahadhari ya wale MWEZI Machi kila mwaka ni mwezi wa wanawake kutokana na kuwa Machi 8 ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo wanawake wanakutana katika maeneo mbalimbali kushereheka na kujadili masuala kadhaa kwa mustakabali wao.
Kati ya mambo ambayo wanawake wamekuwa wakijadili ni pamoja na mafanikio na changamoto zinazowakabili huku wakiangalia fursa mbalimbali zilizopo katika kujiletea maendeleo.
Kipindi hiki wanawake hukusanyika kujadiliana na kufurahi kwa pamoja na ndio maana kumekuwa na taasisi na hata watu binafsi wakiandaa makongamano na majadiliano mbalimbali na kuita wataalamu na wanasaikolojia kwa ajili ya kuzungumza na wanawake masuala ya kujijenga.
Wanawake wamekuwa wakipata fursa nzuri duniani na kuongeza uelewa na kufurahi kwa pamoja na kufahamiana na hata kusaidiana.
Wito wangu wanawake watumie vema mwezi huu kwa kukutana na wanawake wenzao ili kubadilishana mawazo na kamwe wasikubali kukaa ndani tu bila kukutana na wengine kwani itawasaidia kufahamu masuala mbalimbali mapya. Kwa wafanyakazi katika maofisi itasaidia kupata fursa mbalimbali zitakazowezesha kuongeza kipato na hata wafanyabiashara kupata masoko mapya ya bidhaa na masuala mengine yatakayowasaidia kuboresha bidhaa.
Hata kama huwezi kushiriki katika maeneo yanayotaka kuchangia fedha kidogo vipo vyama vinaandaa vitu kama hivyo bila kulipia, ili mradi hakikisha mwezi huu unapata jambo jipya kwa maendeleo yako.
Lakini pia ni vema kama wanawake, walezi wa familia katika makusanyiko yetu kujadili kwa pamoja namna ya kuwalinda watoto dhidi ya vitendo mbalimbali vinavyowaathiri kama kubakwa na kunajisiwa.
Lakini pia kupambana na kukemea mila na desturi zinazoingizwa kutoka nje, hivyo liwe jukumu muhimu kwa wanawake kujadili na kuhakikisha tunawalinda vijana ili wasiingie katika vitendo vibaya vinavyoingizwa kutoka nje.
Ikiwa wanawake kwa kauli moja tutapata ufumbuzi wa masuala haya na ukatili mwingine itakuwa na maana ya maadhimisho ya mwezi huu kwa wanawake na kila mwanamke atajivunia. Ni vema kila mwaka kuwa na mambo ya kujadili na kupata ufumbuzi wa pamoja wa jambo linalosumbua familia, jamii na nchi na siyo kila mwaka kufanya maadhimisho yakishapita basi tunasubiri mwaka mwingine.
Kila la kheri wanawake wote katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, tufurahi, tujadili changamoto zinazotukabili lakini pia tufurahie mafanikio tuliyopata na kuongeza juhudi katika mapambano ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Ni vema kila mwaka kuwa na mambo ya kujadili na kupata ufumbuzi wa pamoja wa jambo linalosumbua familia, jamii na nchi na siyo kila mwaka kufanya maadhimisho yakishapita basi tunasubiri mwaka mwingine.
“ walio karibu nawe wasisikie mazungumzo yako kwani waweza kupata taarifa zako za siri usizokusudia wao kuzifahamu,” mwongozo unasisitiza.
Inasisitizwa mtumiaji kuepuka kupayuka anapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu, mfano benki, maeneo ya ibada na tafakuri, hospitali, kwenye mikutano, darasani.
Mwongozo unasema kwa kawaida, sauti ya mtu anapozungumza na simu inakuwa ni ya juu tofauti na mazungumzo ya ana kwa ana.
Hivyo inashauriwa mtumiaji akitaka kutumia simu kwenye hadhara, akae mbali na watu wengine, angalau hatua nne kutoka mtu wa mwisho kwenye mkusanyiko huo au kama ni kwenye chumba, ni vyema zaidi akitoka nje ya chumba husika.
Vidokezo vingine muhimu ambavyo TCRA inasisitiza watumiaji wa simu kuzingatia ni kuweka mlio wenye staha na heshima kwenye simu kwa kuzingatia maadili ya hadhara/ jamii inayokuzunguka.
Inashauriwa kutotumia simu kwenye maeneo hatarishi yanayoweza kukufanya mtu asahau anachofanya. Kwa mfano, wakati wa kuendesha gari au mitambo, jikoni, kutembea barabarani.
Lakini pia inashauriwa kutotumia simu katika mazingira yanayoweza kuwapa nafasi watu wenye nia mbaya kufanyia mhusika uhalifu. Mamlaka inasisitiza watumiaji kuzingatia masharti ya matumizi ya simu, kwa mfano wakiwa ndani ya ndege, maeneo nyeti n.