KWA mujibu wa tetesi za usajili barani Ulaya klabu ya Paris Saint-Germain-PSG inataka kumsajili nyota wa Barcelona, Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 17 kwa gharama kubwa zaidi katika historia ya soka.
Miamba hiyo ya Ufaransa inayonolewa na kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique, ipo katika mchakato wa kujenga kikosi kwa ajili ya baadaye. (Caught Offside)
SOMA: Arsenal yaingilia usajili wa Nico Williams
Manchester United inamfuatilia kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton kabla ya uwezekano wa kuwasilisha ombi kumsajili Januari, 2025.
Mchezaji huyo anaonekana kuwa mbadala wa Christian Eriksen. (TEAMtalk)
Arsenal inafikiria uhamisho wa nyota wa Barcelona, Arnau Pradas,18.
Kinda huyo amekuwa kivutio kwa maskauti wa Arsenal kutokana na kiwango bora hivi karibuni katika kikosi cha Barca cha vijana chini miaka 19. (Mundo Deportivo)
Barcelona na Atletico Madrid zimeonesha nia kumsajili Thomas Partey mara mkataba wake kumalizika Arsenal majira ya kiangazi 2025. (Fichajes)